GET /api/v0.1/hansard/entries/442877/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 442877,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/442877/?format=api",
"text_counter": 147,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "na nyapara wa kumlinda kila siku kwamba apate usalama. Ni jukumu la kila mwananchi nchini kujua kwamba uzalendo sio kuongea tu lakini ni kutekeleza na kuonekana kwamba ameutekeleza uzalendo ule na akatunza sifa na maisha ya mwenzake. Iwapo mwenzako ameingiliwa na majambazi ilhali wewe umenyamaza husemi chochote na upo karibu, unangoja askari atoke Nairobi kilomita 300 aje akufikie wewe na akuokoe ? Haifai ! Kwa hivyo, ninafikiri tunahitaji mafunzo kwa wananchi wa nchi hii kuanzia daraja la mashinani, elimu ya msingi, kidatoni, mpaka hata chuo kikuu. Wanahitaji mafunzo ya uzalendo; kwamba kila mtu ni askari ambaye ana wajibu wa kuitunza nchi yake, kugharamia utunzaji wa nchi yake na kuleta usalama nchini. Na hilo lisipotekelezwa hivyo--"
}