GET /api/v0.1/hansard/entries/442881/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 442881,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/442881/?format=api",
"text_counter": 151,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Bule",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1029,
"legal_name": "Ali Abdi Bule",
"slug": "ali-abdi-bule"
},
"content": "Asante, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii ili nizungumzie jambo hili muhumi katika Kenya hii siku hii ya leo. Mimi binafsi ninavyofikiria ni kwamba viongozi na wananchi wa kawaida nchini Kenya wamekosa uzalendo. Kukosa uzalendo husababisha mtu afanye jambo lisilofaa ndani ya nchi yake. Mkenya akimuua au kumuathiri Mkenya mwingine, huyo si mzalendo. Tumesikia kwamba kule Wajir wananchi wanauana, kule Mpeketoni wananchi wanauliwa, viongozi wanauliwa Mombasa na watu kuuwana ovyo ovyo, lakini hatujaona hatua madhubuti ambayo imechukuliwa hadi sasa. Haya yote ni kwa sababu ya watu fulani kulala kazini. Maseneta, Wabunge, Mawaziri na polisi wote wamelalia kazi zao. Hii ni kwa sababu katika hii Seneti na katika Bunge la Kitaifa, kuna kamati ambazo zinashughulikia mambo ya amani na usalama wa Wakenya. Wakenya wamekuwa wakikosana hapa na pale miaka nenda, miaka rudi, na kamati hizo zimebuniwa kuangalia maslahi ya Wakenya wanaozozana hapa na pale. Katika kamati hizo, hakuna hata siku moja - mimi nikiwa katika kamati ya Seneti ambayo inalipwa kutokana na ushuru wa Wakenya – ya kuenda kuwajulia Wakenya ni nini inasababisha tatizo hili ilhali kila mara tunaenda kumtembelea Rais katika Ikulu na kumwambia kwamba tunafanya kazi. Huo ni ulaghai na kudanganya Wakenya. Nikiumwa na kichwa, mwili wote unadhurika. Mtu akikosa akili hawezi kuwa na fahamu. Kichwa cha taifa la Kenya kina ugonjwa. Sisi viongozi ndio watu wa kulaumiwa. Sisi ndio tumekosa---"
}