GET /api/v0.1/hansard/entries/442891/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 442891,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/442891/?format=api",
"text_counter": 161,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Bule",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1029,
"legal_name": "Ali Abdi Bule",
"slug": "ali-abdi-bule"
},
"content": "Bw. Naibu Spika, nikisema “vichwa” ninamaanisha kuwa katika Kenya hii kuna kiongozi ambaye ametoka Tana River na anawakilisha watu wa Tana River. Kuna yule anayetoka Wajir na anawakilisha watu wa Wajir. Kwa nini tusizungumze hata siku moja kuhusu mbinu za kusuluhisha tatizo hili? Kwa hivyo, tusilaumu yeyote yule kwa sababu sisi tulioko uongozini hapa tumelala kazini. Mimi nikiwa mmoja wa wanachama wa Kamati ya Uwiyano na Nafasi Sawa ambayo inafaa kuhakikisha kwamba Wakenya hawadhulumiwi, ninajua kwamba hatujachukua hatua ya kufika kule. Kwa nini tunaruhusu Wakenya wauane? Bw. Naibu Spika, kwa hivyo, Wakenya kuanzia kwa polisi na hata sisi viongozi tumekosa uzalendo. Polisi wengi wako vyuoni wakisomea shahada za Degree ili waongezwe mishahara. Tunafaa kuwaajiri kazi polisi ambao hawajasoma sana ili wapambane na uhalifu. Masomo mengi ndio yamefanya tuwe na shida Kenya. Tunafaa kuajiri polisi spesheli katika kila kaunti ili wadumishe usalama katika kaunti zao."
}