GET /api/v0.1/hansard/entries/442988/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 442988,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/442988/?format=api",
"text_counter": 258,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Chelule",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13126,
"legal_name": "Liza Chelule",
"slug": "liza-chelule"
},
"content": "Asante sana, Bi. Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi ili nichangia Hoja hii. Nilikuwa na huzuni sana nilipotazama katika magazeti jinsi vijana walivyochomwa na kuuawa. Tunapoongea, ningependa kuomba wenzangu viongozi wa Kenya tuongee tukiwa na nia moja ili tupate suluhisho la mambo ambayo yanaleta shida katika nchi yetu. Bi. Spika wa Muda, ninaunga mkono wale viongozi wanaosema kwamba inafaa wakutane kwa mazungumzo. Inafaa wazuru maeneo ambayo yana shida. Ni lazima uchunguzi ufanywe ili kutambua ni nini inaleta mizozo katika jamii mbalimbali. Kama viongozi wa taifa hili tunakaa Nairobi kwa muda mrefu sana bila kurudi nyumbani na kuchunguza shida za watu wetu. Ni aibu kuwa kiongozi katika taifa ambalo watu wanauawa kama kuku. Nilipotazama nilihuzunika. Ni jukumu letu kama viongozi, kando na majukumu yetu ya kutengeneza sheria na kutetea haki za kaunti, kuhakikisha kwamba kuna usalama kwa sababu hatuwezi kutekeleza hayo majukumu bila amani. Bi. Spika wa Muda, amani ni ya maana sana. Ni jukumu letu kama viongozi katika nchi yetu ya Kenya kuona kwamba kuna amani bila kujali chama au jamii. Hilo jukumu letu sisi pamoja na viongozi wa makanisa na wale wengine walioko mashinani ambao ni lazima tuwahushishe katika kuleta usalama nchini. Ndani ya Seneti hii na Bunge la Kitaifa, kuna kamati zinazohusika na mambo ya usalama. Inafaa tuwe na mkutano ili tupange jinsi tunavyoweza kutembelea wananchi wetu ili tujue shida zao. Hatuwezi kuketi katika Seneti na kusema kwamba tunawakilisha wananchi wa Kenya ikiwa hatuwezi kujua shida zao. Huwezi kusema kwamba wewe ni kiongozi ikiwa huwezi kujua shida za watu ambao unawakilisha. Usalama ni jukumu letu. Tusiwe watu wa kulaumiana kwa sababu ni jukumu letu kama Maseneta kutembelea zile sehemu ambazo zimeathirika ili tufanye uchunguzi. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}