GET /api/v0.1/hansard/entries/442994/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 442994,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/442994/?format=api",
"text_counter": 264,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kisasa",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13124,
"legal_name": "Mshenga Mvita Kisasa",
"slug": "mshenga-mvita-kisasa"
},
"content": "Asante, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii. Mambo yaliotokea Mpeketoni ni ya kuhuzunisha sana. Wanaume na vijana wetu ambao tulikuwa tunawatarajia kutupatia vizazi vijavyo waliuawa bila sababu yoyote. Bw. Spika wa Muda kama Wakenya tunafaa kujua kuwa tuna shida. Kama hujui tatizo huwezi kujua vile utalitatua. Je, shida ipo na kama ipo ni nini? Je, usalama ni polisi ama Bw. ole Lenku? Usalama ni jukumu letu sote. Tusiangalie mtu mmoja peke yake wala tusitarajie malaika aje atuhakikishie usalama wetu. Ni lazima sote tuangalie mambo ya usalama. Kama wenzangu walisema, ni lazima usalama uanzie kule chini mashinani. Tukitarajia usalama utoke katika ofisi ya juu kabisa, basi hatutaupata. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}