GET /api/v0.1/hansard/entries/443000/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 443000,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/443000/?format=api",
    "text_counter": 270,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kisasa",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13124,
        "legal_name": "Mshenga Mvita Kisasa",
        "slug": "mshenga-mvita-kisasa"
    },
    "content": "Bw. Spika wa Muda, nilikuwa nasema kuwa hatufai kuwalaumu magaidi wa Al Shabaab kwa maovu yote. Ni lazima tuwe macho zaidi ili tusiwalaumu tu bila kuchunguza zaidi. Bw. Spika wa Muda, wanahabari wengine pia waliripoti kuwa watu walikuwa wanaulizwa majina na kutakiwa kukariri aya fulani ya Quran au kuulizwa swali kwa Kisomali. Pia vyombo vya habari vinafaa kutueleza mambo vizuri,. Hii ni kwa sababu wao wakitupatia mambo ya ukweli, basi uchunguzi utakuwa rahisi kwetu. Bw. Spika wa Muda, hatuna Kenya nyingine ambayo tutaikimbilia. Kenya ni yetu na ni lazima tuitunze sisi sote. Hakuna nchi nyingine ambayo itatuchukua sisi sote ikiwa nchi yetu itachomeka. Ni lazima tuungane sisi sote kama Wakenya na kutatua shida zetu. Nchi yetu imejaa taharuki na kila mtu ana uoga. Ukiangalia picha za wale vijana ambayo waliuawa ni za kuhuzunisha sana. Si jambo la kufurahisha. Natumai kwamba Mwenyezi Mungu yuko macho. Kile unachofanya leo ujue kuwa utajibu kesho. Asante, Bw. Spika wa Muda."
}