GET /api/v0.1/hansard/entries/443344/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 443344,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/443344/?format=api",
"text_counter": 169,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Machage",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 179,
"legal_name": "Wilfred Gisuka Machage",
"slug": "wilfred-machage"
},
"content": "Bw. Naibu Spika, namshukuru sana Sen.Halima kwa Hoja aliyoileta katika Bunge hili. Kuna mengi ya uchungu ambayo wakati mwingine ni magumu kuyataja na kuyazungumza hapa. Wakati mwingine ukizifikiria zile sehemu zilizosahaulika tangu siku za ukoloni mpaka sasa, badala ya kulia utaangua kicheko, kwa sababu si jambo ambalo halijajulikana na Serikali wala kudhihirika. Nafikiri hili ni jambo ambalo limetendwa kwa nia ya kuua utu wa Wakenya wengine nchini. Wakati umefika ambapo sisi, hasa wale tunaotoka sehemu hizi ambazo sasa wameziita “ marginalized” kwa kimombo, kwenda kotini. Tutaenda kotini tukidai riba kwa dhulma ambayo tumetendewa na Serikali hizo zote mpaka leo. Tumenyimwa haki zetu za kiutu. Sasa hivi ukiwasikia wenzangu wakisema “Oh! Msifikirie ni nyinyi peke yenu; hata wale ambao wameshapewa nafasi, ukienda kwao pia wako na maskini ambao wamesahaulika.” Hii ni kusudi Hoja kama hii ikipita, chochote kile kitakachopatikana, tena wakichukue wapeleke huko kwao. Huu ni ukoloni mambo leo. Hii ni desturi ambayo imeimarishwa ili The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}