GET /api/v0.1/hansard/entries/443346/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 443346,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/443346/?format=api",
"text_counter": 171,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "kuhakikisha kwamba wenzetu nchini Kenya wanaotoka sehemu fulani wamelaaniwa kuwa vijakazi kuwahudumia wengine nchini kwa sababu ya kunyimwa haki zao. Sen. Halima, yualia akinukuu kipengele cha Katiba cha 56 ambacho kweli chatupa haki kuangalia kwa undani ili tupewe haki zetu za kielimu na kiuchumi. Maneno hayo yameandikwa katika Katiba na ameyanukuu kikamilifu. Hili hata si jambo la kulia; macho yangeangazwa Kenya nzima kuona kwamba jamii za hapa na kule zilizonyimwa hizi haki tangu zama hizo wanapewa haki zao. Wakati huu, ukitaka kuona kwa gazeti wakitangaza mambo ya ajira, wanajiuliza ni wangapi watatoka katika sehemu yangu kuja kupata ajira hizo. Lakini mimi nauliza ni wangapi watatoka katika sehemu za Kisomali, Wapokot, Waturkana, na kadhalika, kuja kupata ajira hizo? Wale watakaofaulu kupata kazi hizo zilizotangazwa katika gazeti leo ni walewale waliotoka sehemu ambazo zimemwagiwa na kutunukiwa bahati ya kupata kila kitu nchini. Sisi wengine tunaambiwa: “Hakuna kazi” kwa sababu hauna kisomo cha kutosha. Lakini wewe haukupewa nafasi ya kusoma na ukanyimwa haki zako. Shule iko wapi? Mambo haya yanafanyika miaka 50 baada ya Uhuru. Sen. (Dr.) Machage asimama hapa na kulia juu ya mambo haya ni aibu. Hapa tunaambiwa shule tatu za mabweni zitajengwa katika kila kata. Lakini kama zitajengwa hakuna walimu wa kutosha, vifaa vya elimu, umeme na maji. Huko watadai tumewapa shule lakini hamutaki kwenda katika hizo shule hizo. Hayo ni magofu yasio na kitu lakini mnasema ni shule. Shule gani hizo? Katika sehemu zingine, utapata ya kwamba tabu zao ni kwamba wako na walimu waliotumwa kwenda huko kupita kiasi wanachokihitaji. Mwenzangu amesema kwamba kuna sehemu moja huko Pokot ambako kuna mwalimu mmoja kwa madarasa sita. Kwangu, utapata kwamba hakuna mwalimu isipokuwa yule aliyeajiriwa na wazazi katika madarasa yote manane. Shule hiyo yaitwa shule, ilhali mitihani ya kitaifa ikitolewa, shule hiyo inapewa mtihani sawa na watahiniwa wa Nairobi na Mombasa. Halafu wanawauliza maswali juu ya uwanja wa gofu. Je, uwanja wa gofu una upana na urefu upi? Mwanafunzi wa sehemu hizi hawajahi kuuona uwanja huo. Utaambiwa kuwa huo ndio mtihani, na lazima uupite ndio uende shule ya upili au vyuo vikuu. Juzi niliona wamejaribu wakasema wamepunguza nukta moja ikiwa wewe ni msichana. Na ukiwa kijana, ujue una nukta moja zaidi, lakini wamesahau kwamba katika hizi sehemu zilizoathirika na ambazo hazina vifaa kabisa, mwanafunzi aliyepata gredi ya “C+” anamzidi kiakili yule aliyepata gredi ya “A” katika hizo sehemu zingine. Mwanafunzi huu asipofaulu anaitwa mjinga na analaaniwa na hatajiunga na chuoni kikuu. Labda atakuwa mnyapala au mpishi akiwa na bahati siku zijazo. Asipokuwa na babati, pengine atarudi kijijini, achomwe na miiba akichunga mifugo, awe mwezi na misho wake apigwe marisasi. Hiyo ndio laana ya kutoka mahali wanapoita marginalized kwa Kiingereza sanifu. Hizi ni sehemu zilizonyimwa haki na utu. Kwa hivyo, tusije hapa kutoa machozi ya mamba hapa na huko tunawakandamiza wenzetu. Ukienda Muthaiga, utapata kuna vijiji. Humo vijijini, ni akina nani utawapata huko? Utawapata Wamaasai, Wakuria na wale ambao hawakupata haki zao kielimu. Hawa ndio utakaowapata huko vijijini wakitoa huduma kwa watu wa Muthaiga, Karen na kadhalika. Hao ndio wazalendo wa nchi hii. Twaambiwa “wananchi wa Kenya, unganeni pamoja ili tujenge taifa.” Taifa gani? Ingawa Katiba imetoa nafasi kuangalia hujuma hizi za haki za kibinadamu, yalioandikwa si elimu tu, bali ni lazima mtoto apate elimu ya juu na yenye maana. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}