GET /api/v0.1/hansard/entries/443348/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 443348,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/443348/?format=api",
"text_counter": 173,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Bw. Naibu Spika, hata wanapopanga mipango ya bajeti ya mwaka huu, utaona mipango ya gharama ya utumishi wa Serikali yamesomwa na tumeletewa bajeti hiyo hapa juzi juzi, lakini hatukuona ni kipi kilichotengewa zile sehemu ambazo zilisahaulika. Mungu si Athumani, amefungua hizi sehemu zingine na sasa zimepata madini, mafuta na kadhalika. Sasa twawasikia wakisema “Oh, sasa sisi twaja kuchimba mafuta;” lakini sasa mtaachwa na haki gani? Hata kupata mtu kuajiriwa sehemu hizo ni nadra kwa sababu watu wengi hawajasoma. Huo ndio ukweli ulioko nchini. Huo ndio ukweli wa Serikali zote zilizopita. Sijui kama hii Serikali ya Jubilee pia itamaliza kipindi chake na huo ukweli. Hizi ni laana zisizokuwa na maana kwa jamii, wazalendo na wananchi Wakenya kwa kunyimwa haki hizi."
}