GET /api/v0.1/hansard/entries/445392/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 445392,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/445392/?format=api",
    "text_counter": 296,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "mazao. Lakini mbegu hii huwa na bei ya juu zaidi. Kwa hivyo, watu wengi huwa hawawezi kuinunua. Lakini kama Serikali inaweza kusaidia ili kuhakikisha kwamba mbegu ile itatumiwa kwa sababu ardhi yetu iko sawa na pia hali ya hewa iko sawa. Hivyo basi, tukiupanda mti huu, tutapata manufaa kwa haraka zaidi na watu pia wataweza kujiendeleza haraka zaidi. Kwa hivyo, Bw. Spika wa Muda, tukiangalia haswa katika upande wa kuhakikisha kwamba yale mazao yametokezea, yanaweza kupelekwa hata nje ama katika miji yetu, kwa sababu saa nyingine unaenda upande wa Kaloleni ndani au Kwale ndani, unaona kwamba miti imekomaa, lakini yale madafu yamekaa pale muda mrefu sana mpaka yamekuwa nazi, mengine yameanguka yenyewe. Hii ni vibaya kwa sababu uchumi wetu utazoroteka kwa sababu matunda yale yangetumiwa kuinua hali ya uchumi ya watu wale. Kwa hivyo, iwapo Serikali itaweza, ihakikishe kwamba katika upande wa soko, masoko yawe yapo. Kwa upande wa kutafuta vifaa vinavyoweza kutengezwa kutokana na tunda hili – vitu kama vya kuweka maridadi, urembo na mambo kama haya – yanaweza kupelekwa hata nchi za nje. Kuna watu wengi ambao wakija Pwani, wanafurahia na wangependa kukumbuka Pwani kwa kubeba vitu kama mikeka na bangili zilizotengenezwa kutokana na mnazi ili waweze kutumia na kukumbuka safari yao Pwani. Jambo hili likifanyika, litasaidia sana kwa kuhakikisha kwamba watoto wetu wanaenda shule na kuhakikisha kwamba mambo haya yanayowekwa yanatolewa. Bw. Spika wa Muda, ni muhimu pia kuwe na jina lililowekwa katika vile vifaa vilivyotengezwa kutoka kwa mnazi ili watu wajue kwamba hizi ni bidhaa za mnazi kutoka Kenya. Kwa hivyo, ni muhimu kuhakikisha kwamba pesa fulani zimetengwa kwa ajili ya kuendeleza ukuzaji wa mnazi. Sen. Ongoro amesema kwamba ni muhimu kwamba pesa zitengwe ili kuhakikisha kwamba watu wamepata nguvu na motisha ya kuendelea kuukuza mmea huu. Bw. Spika wa Muda, ningependa kuleta mabadiliko katika Hoja hii. Ukiniruhusu, ningependa nitoe mabadiliko haya kwa njia ya kimombo kwa sababu ya kunukuu, kwa sababu Hoja yenyewe imeandikwa kwa Kimombo. Mabadiliko yenyewe ni haya."
}