GET /api/v0.1/hansard/entries/445889/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 445889,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/445889/?format=api",
"text_counter": 102,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Gathogo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2715,
"legal_name": "Esther Nyambura Gathogo",
"slug": "esther-nyambura-gathogo"
},
"content": "Mhe. Naibu Spika wa Muda, kama ingekuwa wakati wa siasa ningesema kwamba kuna mtu amenikanyangia. Lakini nataka kuongea kuhusu barabara ambayo imetoka Ruiru na kupitia maeneo matatu ya uwakilishi Bunge. Barabara hiyo imetuletea aibu sana sisi Wabunge watatu wa Kaunti ya Kiambu. Hii ni kwa sababu kila wakati ndizi hupandwa katika barabara hiyo kana kwamba ni shamba. Ninashukuru kwa Kshs5 milioni ambazo zimetolewa. Walakini hii ni madharau.Tunaomba barabara hiyo ambayo inatoka Ruiru hadi Githunguri na inaguza eneo la Mburu Kahangara iweze kupewa pesa yakutosha ili iweze kujengwa vizuri na watu wetu wafurahie."
}