GET /api/v0.1/hansard/entries/44612/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 44612,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/44612/?format=api",
    "text_counter": 261,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Mbuvi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 80,
        "legal_name": "Gideon Mbuvi",
        "slug": "gideon-mbuvi"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, shida yao ni kwamba ile tarehe wanayoahidi kuleta taarifa hawaileti. Wanaleta taarifa wakati Mbunge ambaye ameiitisha hayuko Bungeni. Kwa mfano, tarehe 12.5.2011 niliitisha taarifa kutoka Afisi ya Naibu wa Waziri Mkuu na Waziri wa Serikali za Mitaa kuhusu vibanda ambavyo vilijengwa na CDF ya Makadara vya akina mama wauzaji mboga, ambao hawajiwezi. Hivyo vibanda vilivunjwa na wezi – maharamia waliokodishwa na City Hall. Taarifa hiyo ililetwa jana kama simo ndani ya Bunge. Waziri aliahidi kuileta taarifa hiyo tarehe 19.5.2011 lakini hakuileta siku hiyo. Kwa hivyo ninaomba taarifa hiyo iletwe tena Bungeni."
}