GET /api/v0.1/hansard/entries/44662/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 44662,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/44662/?format=api",
    "text_counter": 311,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Kuttuny",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 61,
        "legal_name": "Joshua Serem Kutuny",
        "slug": "joshua-kutuny"
    },
    "content": "Ninakushuru sana, Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa nafasi hii. Ni jambo la kusisitisha sana kuwa Bw. Waziri hayuko tayari kutoa arifa kutoka kwa Wizara yake juu ya jambo hili. Wiki jana aliahidi kutoa arifa katika Bunge hili juu ya jambo hili kwa sababu ni muhimu sana kwetu. Hii ndio hospitali inayotoa huduma za afya kwa watu wengi. Ni aibu kuona huduma inatatizwa na vifo vingi vinatokea katika hospitali hii. Hakuna dawa za kutosha katika hospitali hii. Vitendo vya Waziri vimechangia pakubwa katika upungufu huu wa huduma. Taharuki imetanda katika hospitali hii kwa sababu wafanyakazi wengi tayari wamepokea barua za kuwasimamisha kazi. Je, ni nidhamu kwake kusema tusubiri arifa hii hadi tarehe 7/06/2011 na ilhali alikuwa ametuahidi kuitoa hivi leo?"
}