GET /api/v0.1/hansard/entries/447311/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 447311,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/447311/?format=api",
"text_counter": 316,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Dr.) Shaban",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 139,
"legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
"slug": "naomi-shaban"
},
"content": "Ahsante sana, Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii ya kumuunga mkono kiongozi wetu wa waliowengi hapa Bungeni. Wakati umefika wa sisi kuelekea kwenye likizo kwa muda huu wa siku kumi ambazo tunahitaji kurudi kwa wale ambao walitupatia jukumu hili la kuja hapa ili tuweze kuwazungumzia na kuwapatia masaa yetu haswa kwa maswala yale ambayo tumekuwa tukiwatumikia. Tangu pale mwanzo, kuna umuhimu wa sisi kuenda kukaa na wananchi. Naibu Spika wa Muda na hata sasa hivi, tunafahamu ya kwamba pesa za hazina ya maendeleo kule mashinani na haswa kwenye maeneo Bunge, zimetoka. Orodha yenyewe imetoka leo na wakati ni sasa wa sisi kuweza kukaa na kamati zetu na pia kuenda kuwahamasisha wananchi. Naibu Spika wa Muda, tuna majukumu kadhaa. Hapo awali nilikuwa Waziri wa Mipango Maalum kwenye Ofisi ya Rais na niliona mateso yale Wakenya walipitia. Wakati huu, ningeomba ndugu zangu wote tukirudi mashinani kule maeneo Bunge tuweze kuwazungumzia wananchi kuhusu umuhimu wa amani na umuhimu wa umoja wa Kenya. Naibu Spika wa Muda, nikiendelea kuunga mkono---"
}