GET /api/v0.1/hansard/entries/447338/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 447338,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/447338/?format=api",
"text_counter": 343,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Kimaru",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2072,
"legal_name": "Anthony Mutahi Kimaru",
"slug": "anthony-mutahi-kimaru"
},
"content": "Ahsante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda. Ningependa kuchangia Hoja hii ya kuwapa Wabunge likizo ya muda, ili tuweze kwenda mashinani na tuweze kuwa na wenzetu kule. La muhimu zaidi ni kuhusu fedha za CDF ambazo, kwa hakika, mahali pake sio kwenye benki, bali zinafaa zitolewe. Tayari tumeshapata zile fedha. Ziweze kutolewa na kuwafikia wananchi. Miradi yote kule ambayo imepewa pesa, ni wakati wa kwenda kutoa zile hundi za pesa, ili miradi yote ambayo iko kule iweze kuendelea barabara. Vile vile, ningependa kusema kwamba wakati huu ambao tunaenda likizoni, tumepitisha Ripoti ya kuwa na halmashauri za kusimamia maendeleo katika kaunti. Hili ni jambo nzuri sana na litawezesha kuweko na uwajibikaji ili maendeleo yafike kule mashinani na kuzuia ufujaji wa pesa. Wakati ambao hatukuwa na halmashauri, tuliweza kupata kwamba fedha hazikutumika kwa njia mwafaka. Fedha nyingi zilitumika vibaya. KERRA ilikuwa inafanya barabara moja na ile barabara pia, kaunti nayo ilikuwa inazingatia kuijenga. Kukiwa na jambo kama hilo, ni kuonyesha kwamba kuna fedha fulani ambazo hazikutumika vizuri. Tukiwa na mikakati kama hiyo, kwa hakika, tutaweza kupata maendeleo ya hali ya juu. Mwaka uliopita wa fedha za Serikali, kulikuwa na fedha ambazo zilitengwa za kuwaajiri wauguzi na wafanyi kazi wa afya. Sijaona jambo kama hilo likifanyika kule kwetu. Nadhani katika nchi yote, hakuna mahali wauguzi waliajiriwa. Tunashangaa hela ambazo zilitengwa zilienda wapi. Inafaa tuwe na amani tunapoelekea likizoni kwa sababu amani ni muhimu sana. Hata ndugu zetu wakitaka kwenda katika Uwanja wa Uhuru Park wapewe nafasi. Lakini nao wakifika pale, wahubiri amani kwa sababu mambo yakuchezea shari amani ya nchi yetu ni jambo ambalo halitaruhusiwa na halifai kuruhusiwa. Lakini kama---"
}