GET /api/v0.1/hansard/entries/447645/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 447645,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/447645/?format=api",
"text_counter": 294,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "tumekuwa na shida. Shida hii haijatokea tu kule Pwani bali katika mambo yote ya ukulima. Bw. Spika wa Muda, ni bahati mbaya sana kwamba mambo ya ukulima yameachiliwa ilhali ni uti wa mgongo wa uchumi wetu. Asilimia 80 ya watu nchini Kenya wanategemea ukulima. Haswa kule Pwani asilimia 90 ya watu wanautegemea mnazi. Kama vile Sen. Karaba alisema, kuna mimea mengine ambayo watu wamejaribu kupanda kule Pwani. Watu wamejaribu kupanda mimea kama mihogo na mahindi lakini haijanawiri kama mnazi. Bw. Spika wa Muda, mnazi ni mti wetu wa Pwani wa maisha. Ni mti ambao Mungu ametupatia ili tuweze kuutumia. Mtu yeyote ambaye amefika Pwani ameona ile kazi ambayo mnazi umefanya. Mpwani yeyote anapopika chakula, mpaka akitie nazi. Chakula hakisemekani kama ni kitamu mpaka kitiwe nazi. Bw. Spika wa Muda nyumba nyingi za watu wa Pwani zimewekwa makuti. Hata vile vigogo ambavyo vimewekwa upande wa ukuta, pia vinatoka kwa mti wa mnazi. Makuti hii imetumika hata katika hoteli. Lakini kwa miaka michache iliyopita ni kama biashara hiyo imerudi chini. Kitambo kidogo ungeweza kuona hoteli nyingi kubwa ambazo zimejengwa kwa makuti. Kuna mahali karibu na Serena panapoitwa Makaburini. Miaka 10 iliyopita ungewaona wanawake wa Kigiriama wakiuza makuti yao pale. Lakini siku hizi, hatuoni mambo kama haya yakifanyika. Kwa hivyo, huu ni mmea ambao umesahauliwa kabisa. Hii ina maana kwamba watoto ambao wangeweza kusoma hawatasoma. Elimu ni nadra sana upande wa Pwani. Watoto wengi hawaendi shuleni kwa sababu ya ukosefu wa karo. Serikali inajua kwamba mmea huu ni mmea wa maisha haswa kwa Wapwani, lakini machache sana yamefanywa kuhakikisha kwamba mmea huu umekuzwa. Ni kweli kwamba mmea huu huchukua muda kukua, lakini ukiangalia manufaa yake haswa kwa uchumi--- Kuna vitu kama mikeka na hata vijiko. Mti huu ni kama baraka kwa watu wa Pwani. Bw. Spika wa Muda, ingekuwa bora sana kama Serikali ingesimamia ukuzaji wa mnazi. Asilimia kubwa ya watu wa Pwani wanaishi katika hali dhaifu kiuchumi. Hii ni kwa sababu wengi wao hawajapata masomo ya juu. Kwa hivyo, wengi wanautegemea mti huu. Sen. Ongoro ametuelezea manufaa ya mti huu. Tuna kinywaji cha madafu ambacho kiko tayari. Tunafaa kukiuza kinywaji hiki hata katika hoteli zetu. Hakufai kuwa na soda za Fanta na Coca Cola tu. Tunafaa kuwa hata na kinywaji cha madafu ambacho kitaonyesha kwamba tunazingatia utamaduni wetu. Lakini utaona kwamba vitu kama hivi haviuzwi katika hoteli. Vinauzwa nje ya hoteli kwa bei ya chini sana ambayo haiwezi kuwasaidia hata wale ambao wanataka kuutumia mti kama huo ili uwe na manufaa kwao. Kwa hivyo, inaonekana kwamba kwa muda mrefu, Serikali pengine hata na wanasiasa wenyewe, hatujatia maanani ule mti vile ambavyo inapaswa. Ndio maana ninataka kumpongeza dada yangu, Sen. Ongoro, kwa kuleta Hoja hii ambayo inaweza kutuwezesha sisi, Wapwani, kuangalia na kusema kwamba huu ni mti wa maana. Hoja hii imechukua muda mrefu kufika hapa, lakini manufaa yake ni muhimu haswa katika Pwani; na ni vipi tutaweza kuukuza mti huu; ni vipi tutaangalia mbinu tofauti tofauti ambazo huu mti unaweza kukuzwa hata kwa haraka zaidi ? Inajulikana sasa kwamba kuna mbegu ya mti huu ambayo sio lazima mti wenyewe ukue mrefu sana; mti wenyewe unakua kwa muda mfupi – karibu miezi sita – halafu unaanza kupata The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}