GET /api/v0.1/hansard/entries/447649/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 447649,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/447649/?format=api",
    "text_counter": 298,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Bw. Spika wa Muda, ni muhimu kwamba Hoja hii imeletwa hapa. Kwa hivyo, yatakikana tusaidie kutafuta suluhisho. Ikiwa twaweza kutafuta suluhisho kama hili ambalo litaweza kusaidia katika manufaa haya ambayo yamelezwa hapa; kwamba yaendelee zaidi kudumishwa na mambo ambayo yamezungumzwa yajulikane; magonjwa ambayo yanaweza kuponywa kwa kutumia maji ya madafu na mambo kama hayo pia yajulikane. Ni muhimu tukiwa na pesa ambazo zitawekwa kando, baadaye tutaweza kuangalia watapata asili mia ngapi. Lakini kukiwa na mikopo fulani wa kitaifa ambayo itahakikisha kwamba ile minazi ambayo itapandwa sio minazi ambayo itashindwa kukua kwa sababu hakukuwa na pesa; sio minazi ambayo itapandwa halafu isiwe na manufaa kwa sababu watu hawawezi kutumia mazao yanayotoka katika mnazi ule. Bw. Spika wa Muda, hili ni jambo muhimu sana kwa sababu hapa tunazungumza juu ya maisha ya watu. Ijapokuwa tunazungumza juu ya uchumi, pia tunazungumza juu The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}