GET /api/v0.1/hansard/entries/450686/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 450686,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/450686/?format=api",
"text_counter": 297,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Machage",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 179,
"legal_name": "Wilfred Gisuka Machage",
"slug": "wilfred-machage"
},
"content": "Asante sana, Bw. Spika. Nikiunga Mswada huu, ningetaka kuwapongeza wale Maseneta watatu waliotuwaakilisha vizuri katika Kamati hii. Ningependa kuwapongeza kwa kazi nzuri waliotekeleza katika kikao hiki cha kuratibisha Mswada huu. Lengo la Mswada huu linadhihirika wazi wazi na haina haja tukumbushane kwa sababu tuliwahi kutoa maoni yetu kuhusu Mswada huu hapo mbeleni. Hata hivyo, Sen. Sang ambaye alipendekeza Mswada huu inafaa ajue kwamba siku huwa na alfajiri, adhuhuri na jioni. Siku njema huonekana asubuhi. Pia siasa nzuri huonekana mapema. Akiendelea hivyo, ninaona siku nzuri imeanza na imedhihirika kwa mawazo yake, katika siasa yake nzuri na mapendekezo yake yenye maana na hekima kwa Bunge hili. Ninaamini ya kwamba Magavana watasoma Mswada huu na kuuelewa vizuri. Ni Mswada wa uwiano na kuleta watu pamoja. Unahimiza kukaa, kufikiria na kutekeleza mapendekezo ya maendeleo mashinani vilivyo. Kulingana na desturi za Waafrika kikao kilicho na mzee kinatosha. Seneta ni mzee wa kaunti kulingana na Katiba yetu. Ni lazima apewe wajibu wake kuwa mwenyekiti wa kikao hiki na kutoa mashauri na si amri, kufuatana na mapendekezo ya viongozi wa mashinani, wakiwemo Wabunge. Bw. Spika, pia ningependa kuwataatharisha kwamba mwisho wa Mswada huu unatoa hukumu kwa yeyote yule atakayefikiria kwamba anaweza kuhujumu kazi hii isitekelezwa kule mashinani. Bw. Spika, naunga mkono."
}