GET /api/v0.1/hansard/entries/450745/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 450745,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/450745/?format=api",
"text_counter": 356,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Njoroge",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13158,
"legal_name": "Ben Njoroge",
"slug": "ben-njoroge"
},
"content": "Bw. Spika, ningependa kukushukuru kwa kunipa nafasi hii. Kwanza, ningependa kuipinga Hoja hii. Licha ya mjadala huu kuwa mzuri, kuweka kando walemavu ambao walichaguliwa kwenye kaunti ni dhuluma na ubaguzi wa hali ya juu. Bodi hii itakapokuwa inakaa, walemavu watakuwa wakiwakilishwa na kina nani? Hii ni bodi ya kaunti ambayo itakuwa ikijihusisha na mambo ya maendeleo. Ikiwa katiba ilipiganiwa na ikapita na tukapewa nafasi hizi, sielewi kwa nini Seneti na NationalAssembly zilifikiria kutunyima nafasi hizo. Ingekuwa afadhali kama tungewaweka walemavu katika Bodi hiyo badala ya kuwaacha nje."
}