GET /api/v0.1/hansard/entries/451369/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 451369,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/451369/?format=api",
    "text_counter": 235,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Gichigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1909,
        "legal_name": "Samuel Kamunye Gichigi",
        "slug": "samuel-kamunye-gichigi"
    },
    "content": "Nashukuru sana Bi. Naibu wa Spika kwa kunipatia hii nafasi. Ningependa kuanza kwa kumpongeza Rais Kenyatta kwa Hotuba yake. Namshukuru kwa kuweza kufika hapa ili kulitangazia taifa yale mambo Serikali ya Jubilee imekuwa ikifanya kwa muda wa mwaka mmoja ambao umepita na yale ambayo Serikali inapanga kufanya kwa kipindi kijacho. Kuhusu maadili ya kitaifa na misingi ya utawala, lile ambalo litafanya hii nchi iweze kuendelea ni sisi kuanza kutilia maanani maadili. Kwanza kabisa inatupasa kushikilia uzalendo. Isiwe kwamba kila mtu anajitakia mambo yake binafsi na kusahau mambo ya taifa. Ukienda kwenye barabara, kila mmoja anataka kuruka laini ili aweze kufika mbele ya watu wengine na hali wanavunja sheria. Ukienda kwenye biashara hasa na Serikali kila mmoja anajaribu kutoa hongo ili aweze kupitishwa mbele ya wengine ambao wangefaulu zaidi. Kuhusu umoja katika nchi, nafikiri kwamba ni muhimu sisi Wabunge tuepuke mizozo. Isiwe kwamba tukija hapa kila wakati tunazozana tukijaribu kuonyesha jinsi sisi tuko upande huu na wale wengine upande ule mwingine. Sisi ni viongozi wa taifa na tunastahili kuiweka hii nchi pamoja pasi na kuleta utengano hasa tukitumia ukabila. Ni muhimu pia tuanze kuwakumbuka na kuwaheshimu mashujaa wetu. Tuna mashujaa wengi sana ambao wamepigania hili taifa tangu enzi za uhuru. Kufikia sasa tunaongea tu wala hatufanyi jambo kuwakumbuka mashujaa wetu. Jambo ambalo ningekumbuka na ninafurahi kwamba Serikali ya Jubilee imelifanya ni kuwakumbuka wanyonge katika jamii. Hili jambo la kuwapatia wazee kiinua mgongo ni bora. Tumewakumbuka mayatima. Tumeongeza zile pesa ambazo huwa wanapatiwa. Wale ambao ni walemavu katika jamii tumeweza kuwaongezea pesa. Haya ni mambo muhimu katika nchi. Serikali ya Kibaki iliwakumbuka wanafunzi wa shule za msingi. Itakuwa muhimu sana basi Serikali hii yetu ya Jubilee iwakumbuke wanafunzi wa shule za upili ili wanafunzi wote, kama ambavyo Katiba imenena, masomo ya msingi yasikomee Darasa la Nane, bali yafike Kidato cha Nne. Hivyo, nchi hii itaendelea zaidi. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}