GET /api/v0.1/hansard/entries/454354/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 454354,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/454354/?format=api",
"text_counter": 315,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Kombe",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 250,
"legal_name": "Harrison Garama Kombe",
"slug": "harrison-kombe"
},
"content": "Ahsante Mhe. Spika. Nasimama kuunga mkono Ripoti iliyo mbele yetu ya kuwachagua Makamishina Bi. Kagwiria Mbogori kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Kitaifa ya Haki za Kibinadamu pamoja na wenzake. Pia naunga mkono kukataliwa kwa Bw. Lempaa. Kwa hakika, tuna matarajio kwamba Tume hii itafanya kazi yake vyema. Nimepitia Ripoti hii na nikaona kwamba baadhi ya wahusika hawa wamefanya kazi nzuri sana, hasa kwa kuzingatia dhuluma za kihistoria. Hivi tunavyozungumza, natoka kwa Kamati ambayo imeweza kufuatilia Ripoti ya NEMA, lakini ni dhuluma tupu ambayo imeendelea pale ndani. Mashamba ambayo kwa hakika yanastahili kuwa ya wenyeji yamechukuliwa na hivi sasa, badala ya kuwachiliwa kwa kilimo, yanatumika kupanda miti ilhali wawekezaji hawakuyaitisha mashamba hayo kwa kupanda miti. Waliyaitisha kwa kutengeneza chumvi. Watu wamepigwa risasi katika maeneo hayo wakitetea haki zao. Basi, ni matumaini kwamba Tume hii itaweza kuangazia hasa Ripoti ambayo imeandikwa na Tume iliyotangulia kulingana na mashamba yale ya chumvi na mapendekezo yake yatekelezwe kikamilifu ili watu wa eneo lile la Marereni, Kanagoni na Msumarini waweze kupata mashamba yao. Mhe. Spika, naunga mkono Hoja iliyo mbele yetu ili walio mbele yetu wakaweze kuhudumu katika Tume hiyo. Asante."
}