GET /api/v0.1/hansard/entries/45538/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 45538,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/45538/?format=api",
    "text_counter": 325,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Muthama",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 96,
        "legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
        "slug": "johnson-muthama"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, inafaa Waziri afahamu kwamba Wakenya wanahitaji majengo mazuri na imekuwa kikwazo kikubwa sana kuweza kufanya ujenzi huo. Kikwazo kikubwa sana ni bei ya vifaa vya ujenzi. Ningependa Waziri aangalie sana bei ya simiti. Mfuko mmoja wa simiti sasa ni zaidi ya Kshs800 ilhali simiti kutoka Misri inaweza kupatikana kwa Dola Mbili au Kshs150. Hatujui ni kwa nini bei ni ghali hapa kwetu. Majengo ya kiajabu yametapakaa nchini kwa sababu wananchi hawawezi kujimudu. Jambo la pili ni kwamba wananchi wa nchi hii wametengwa katika kupata kandarasi za kufanya kazi. Utapata kijana ambaye amesoma na kuhitimu na anataka kuanza kazi yake na anapoandikisha kampuni yake na kuweka zabuni yake ili aweze kupata kandarasi, anaulizwa kwanza athibitishe kwamba ana nguvu au pesa, mashini na vyombo vya kufanya hiyo kazi. Kijana aliyetoka shule hatakuwa na vitu hivyo. Kazi itamshinda na itapewa mgeni ambaye amekuja na anajimudu na mashini zake. Mwishowe huyo kijana atakuwa mwizi."
}