GET /api/v0.1/hansard/entries/45539/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 45539,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/45539/?format=api",
"text_counter": 326,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 96,
"legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
"slug": "johnson-muthama"
},
"content": "Jambo la tatu ni kwamba tunataka vijana wetu waliosoma watumiwe kuangalia ndugu zetu ambao wanaanzisha majengo yao bila ujuzi. Kuna wahandisi ambao wanaweza kwenda na kuwakashifu wanaofanya kazi duni. Kwa hivyo ikiwa tumewasomesha watoto wetu na wameajiriwa na Wizara, tunataka watembee wakitoa huduma zao na wasingojee majengo yajengwe halafu yaporomoke na kuanza kuwalaumu waliojenga na kuwaambia kwamba hawana ujuzi wa kutosha. Tunalipa karo kuwasomesha watoto wetu ili wasaidie nchi."
}