GET /api/v0.1/hansard/entries/455829/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 455829,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/455829/?format=api",
    "text_counter": 197,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Dr.) Shaban",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 139,
        "legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
        "slug": "naomi-shaban"
    },
    "content": "Kuhusu idadi ya watu, ukitumia asilimia 45 kugawa pesa, kwa sababu ya wingi wa watu, basi utaendelea kudunisha maendeleo kwenye maeneo hayo kwa sababu huko hakuna watu. katika Taita Taveta pesa zile ambazo tumepatiwa mwaka huu, awamu hii ya kwanza ni Kshs2.8 milioni. Ukiondoa pesa ambazo ni za kulipa wafanyikazi, utaona kwamba pesa ambazo zimebaki ni kidogo. Wenye kutengeneza hii katiba walijua wazi kwamba, kama kutakuwa na makosa kwa sababu asilimia kubwa ya pesa zinapatiwa sehemu kulingana na idadi ya watu, maeneo yaliyo nyuma kimaendeleo yatazidi kuumia. Hii ndiyo sababu wakaona waweke hazina hii ya kusawazisha maendeleo kwenye maeneo hayo. Ni kweli kwamba maeneo haya yasipoangaliwa kwa undani sana na kusaidika katika hazina hii, yatabaki nyuma. Hata hiyo miaka 20 ikiisha, maeneo hayo yatakuwa bado nyuma kimaendeleo. Ukiangalia, maeneo ambayo tayari yana maendeleo kama Nairobi, Mombasa na maeneo yenye watu wengi kama Bungoma, ndiyo yamepata pesa nyingi. Eneo la Turkana pekee ndilo limepata pesa zaidi ukilinganisha na maeneo mengine. Hazina hii imekuja kuokoa wananchi, lakini isipoangaliwa vizuri itatuumiza badala ya kutusaidia. Ningeomba hazina hii itumie maeneo Bunge wala si maeneo ya kaunti. Hii ni kwa sababu utapata mahali kama Homa Bay, kule Mhe. Mbadi na Mhe. Millie Odhiambo-Mabona wanakotoka, kusema ukweli kuna shida; hakuna hata barabara ya lami. Matatizo yao ni kama yale yanayotukabili sisi. Ukienda maeneo ya Baringo, utapata kuna maeneo makame sana na yenye matatizo makubwa; ijapokuwa eneo lote la Baringo unaona lina afadhali, kuna maeneo bunge ambayo yako vibaya sana."
}