GET /api/v0.1/hansard/entries/456977/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 456977,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/456977/?format=api",
"text_counter": 149,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Gichigi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1909,
"legal_name": "Samuel Kamunye Gichigi",
"slug": "samuel-kamunye-gichigi"
},
"content": "Wakati wa siku ya mashujaa mwaka huu niliweza kupata maoni ya wananchi wangu wa Kipipiri kuhusu ni watu gani tunaweza kuita mashujaa katika eneo bunge langu. Kuna watu walitajwa na bila shaka niliona kwamba hatukuwa na utaratibu mzuri wa kuwatambua mashujaa katika nchi yetu. Tangu tupate uhuru, tumekuwa na mpango ambapo vibaraka na viongozi wa Serikali zilizopita walitunukiwa tuzo za ushujaa. Wale wananchi wetu ambao walijitolea kutetea haki zetu na kulinda hii nchi na kuleta mema na utukufu kwa nchi hii, hawakutambuliwa. Wengi wao walikufa wakiwa na shida nyingi. Hatutasahau mashujaa wetu kama hayati mhe. Shikuku, Bildad Kaggia, Seroney na wengine wengi ambao sisi kama Wakenya hatukuwatambua. Kwa hivyo, hii ni Hoja ambayo imeletwa wakati wake. Katika Hoja hii kuna utaratibu mzuri sana wa kuwatambua mashujaa wetu kutoka sehemu mbalimbali na si mashujaa wa kisiasa peke yake. Tuna mashujaa katika michezo, waliopigania uhuru na wengine wengi wa kutambuliwa."
}