GET /api/v0.1/hansard/entries/456994/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 456994,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/456994/?format=api",
"text_counter": 166,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Linturi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 69,
"legal_name": "Franklin Mithika Linturi",
"slug": "franklin-linturi"
},
"content": "Asante sana, Bi. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi hii ili kuweza kuchangia Mswada ambao uko mbele yetu siku ya leo. Wacha nianze kwa kusema kwamba Mswada huu umefika katika Bunge hili wakati unaofaa, na hakungekuwa na wakati mwingine mzuri zaidi kuliko wakati huu, kwa vile mwezi ujao, wakenya watakuwa wanasheherekea miaka 50 tangu Kenya ijinyakulie uhuru kutoka kwa wabeberu. Wakati kama huu nasema ni nafasi njema tukiweza kuupitisha ili kuweza kuwatambua na kuwapatia nafasi ya kuwashukuru viongozi wa aina mbalimbali ambao wamechangia kuileta Kenya yetu kutoka kwa wakoloni mpaka pale tulipofika kwa njia mbalimbali za kiuchumi, kisiasa na hata kibiashara. Kitu kinacho nifurahisha katika Mswada huu ni kwamba sasa tutakuwa na nafasi na njia imewekwa vizuri kutokana na kupitishwa kwa sheria hii kuweza kuwatambua viongozi mbalimbali ambao wamejionyesha ama kujitokeza kama mashujaa kwa njia mbalimbali katika taifa. Hii inatupa nafasi ya kuweza--- Kama wakenya wataweza pia kutoa maoni yao, mtu fulani hataweza kutambulika kama shujaa. Nimefurahi kwa sababu eneo ninalowakilisha la Meru na wale wanaokumbuka na kujua watu wa mwisho kutoka kwa msitu wakati wa kupigania uhuru wa nchi hii, walikuwa watu wa eneo letu. Baadhi yao ni mzee Jenerali Mwariama, Baimungi na wengine. Hawa watu familia zao saa hii ni maskini hohehahe. Ni watu ambao walisema The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}