GET /api/v0.1/hansard/entries/456995/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 456995,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/456995/?format=api",
"text_counter": 167,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Linturi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 69,
"legal_name": "Franklin Mithika Linturi",
"slug": "franklin-linturi"
},
"content": "wangepigana na mbeberu ili waweze kulikomboa taifa na kurudisha ardhi. Lakini vita vilipoisha hata familia za hawa watu mpaka wa leo wanaishi kama maskwota. Hawajawahi kupata chochote. Nafurahi kwamba Mswada huu unatupa nafasi ya kuweza kuwasaidia hata jamii za hao mashujaa. Kwa hivyo, Mswada huu umekuja wakati mwema na naomba kila mtu aweze kuuchangia na kuupitisha kwa sababu historia ndiyo tunaweza kuiandika. Hatuwezi kuwasahau watu kwa sababu wamefanya kazi nzuri; sisi husema kwamba mtu hujizika akiwa hai. Mashujaa wale tutaweza kuwatambua wamefanyia taifa hili kazi muhumi, ya maana na kwa namna ambazo wataweza kutambulika. Ningewaomba pia wakati tunapowaangalia wale viongozi, tuweze pia kuwatambua hata kama wamelala futi sita chini. Hicho kitakuwa kitu cha maana, na ambacho kitaweza kuleta hata mori kwa watu wengine na wajue kuna maana na manufaa ya kuweza kuisaidia nchi, na kuuliza mimi nikiwa Mkenya naweza kusaidia taifa letu kwa njia ngani. Ningetaka kumalizia kwa kusema kwamba tuna nafasi kama Bunge na viongozi wa karne hii kuweza kukumbuka kwamba tulipewa taifa na wale waliotutangulia likiwa limesimama imara. Kama tunataka pia kuwa mashujaa, ni lazima sote tuchangie kujenga taifa letu na tuwe na jukumu kama Wakenya, kila mtu pale alipo, hata ikiwa ni kwa biashara, siasa, injili au jambo lingine lolote. Inafaa tuweze kuhakikisha--- Nafasi zimewekwa hapa za kuweza kuwatambua, tujue kwamba tuna jukumu kama Wakenya la kuweza kuliunda taifa ambalo sisi tunaweza kujivunia katika maisha ya baadaye. Nchi nyingine ambazo nimetembelea, ukienda kwa Bunge zao, ama kwa majeshi yao, utapata watu wote ambao wamefanya kazi, wameweza kutambulika na orodha ya majina yao imewekwa. Huu ni wakati wetu pia kuiangalia historia yetu, na kuweza pia kufanya mambo kama hayo. Asante sana, Bi. Naibu Spika wa Muda; naunga mkono Mswada huu."
}