GET /api/v0.1/hansard/entries/457053/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 457053,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/457053/?format=api",
"text_counter": 225,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Khamisi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 874,
"legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
"slug": "mishi-juma-khamisi"
},
"content": "Ahsante Bi. Naibu Spika wa Muda. Nasimama kuunga mkono Mswada huu. Huu Mswada umekuja wakati unaofaa; wakati ambapo Wakenya tunasherehekea miaka 50 tangu tujikomboe kutoka kwenye minyororo ya wabeberu na kuweza kujitawala kama Wakenya. Mswada huu unatambua na kuteua mashujaa. Wakenya tumekuwa na fikira kwamba mashujaa wa ukombozi wa uhuru wametoka katika jamii fulani ama sehemu fulani humu nchini. Lakini mashujaa wetu wa uhuru wametoka katika Jamhuri yetu yote ya Kenya. Kwa mfano, kule kwetu pwani tunaye mama yetu Mekatilili wa Menza. Yeye alikuwa shujaa ambaye alitembea kilomita 1,200 kwenda na kurudi ili kuwatetea wakenya dhidi ya dhuluma za wabeberu. Tunao watu kama vile Abdalla Bambaulo na Mfalme wa Digo, Kubo. Wao pia walipigania uhuru wetu. Mswada huu utaangalia vigezo na kutengeneza sera ambazo zitaweza kutambua mashujaa ni akina nani. Kuna wale ambao watakuwa mashujaa bandia na hiyo haitakuwa sawa. Iwapo tutakuwa na sera mwafaka, basi tutajua shujaa ni nani. Mswada huu pia umezungumzia vitengo mbali mbali vya mashujaa. Mswada huu pia unatambua mashujaa kupitia uvumbuzi. Labda kuna Mkenya fulani ambaye amevumbua jambo ambalo litawasaidia Wakenya kutatua shida fulani. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}