GET /api/v0.1/hansard/entries/457054/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 457054,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/457054/?format=api",
    "text_counter": 226,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Khamisi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 874,
        "legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
        "slug": "mishi-juma-khamisi"
    },
    "content": "Kuna wale pia watakuwa wameleta maadili fulani katika nchi yetu. Huu Mswada kwa kweli umezungumzia nani ndiye shujaa. Tumekuwa tukifikiria kwamba ushujaa ni wa wale waliopigania uhuru peke yao. Hata hivyo, tunaona kwamba mashujaa wako katika nyanja nyingi sana. Tuna mashujaa hata katika mambo ya elimu. Tuna waalimu na maprofesa ambao wamevumbua hali nyingi. Mfano ni maprofesa wa hesabu ambao wamevumbua formula za kutatua matatizo yetu katika nyanja ya hesabu. Vile vile, tuna mashujaa katika soka. Wengi pale mashinani wamesahaulika. Tunawataja sana wanasoka wa nchi za nje na tunawasahau wetu. Mswada huu ukipitishwa tutakuwa na miundo misingi wa kuwatambua mashujaa wetu. Nimefurahi kwa sababu Mswada huu umezungumzia hazina ya fedha ambazo zitawasaidia mashujaa ama waliokuwa wakiwategemea mashujaa. Mfano hapa ni Dedan Kimathi na Mekatilili wa Menza. Jamii zao ziko katika hali ya umaskini. Iwapo tutakuwa na hazina hiyo, basi itawasaidia wake na watoto wa mashujaa. Lazima pia tuweke vigezo ili tujue fedha hizo zitasaidia kwa njia gani. Tukiacha hazina hii itumike tu wakati shujaa ana mahitaji ya fedha, basi tutakuwa tumeacha mwanya mkubwa sana ambao pengine utatuletea matatizo. Lazima tuseme kwamba fedha hizo zitasaidia, pengine, katika kusaidia jambo fulani. Hivyo, hatutatumia vibaya fedha hizo. Mswada huu utawafanya Wakenya wachanga walioko sasa waweze kuona vielelezo vyema katika mashujaa ambao walipigania uhuru wetu ama kutuletea mambo fulani humu nchini. Mswada huu utaangazia vile vile Wakenya ambao wameleta mageuzi Tulikuwa nchi ambayo ilikuwa na chama kimoja cha kisiasa, lakini kuna wale ambao walipigania demokrasia. Wengine walipoteza maisha yao na wengine walipigania na kuhakikisha kwamba ni lazima Wakenya wawe katika sera ya vyama tofauti ili tuweze kujieleza kisiasa na kufanya siasa huru. Kuna wengi waliopigania mazingira, kama dada yangu marehemu Wangari Maathai. Alipigania sana mambo ya mazingira yetu. Hadi wakati huu, tunafuata njia zake ili kuhifadhi mazingira yetu. Watu kama hao ni lazima tujue watakua vipi kielelezo kwa jamii zilioko sasa ili wengi wao waweze kuingia katika mambo kama hayo."
}