GET /api/v0.1/hansard/entries/457055/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 457055,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/457055/?format=api",
    "text_counter": 227,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Khamisi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 874,
        "legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
        "slug": "mishi-juma-khamisi"
    },
    "content": "Nafurahishwa sana pia na Mswada huu kwa sababu umezungumzia kuhusishwa kwa Wakenya ama jamii katika kutambua mashujaa. Itakuwa vyema zaidi wakati baraza litaundwa ili kuhusisha Wakenya kule mashinani ambao pengine wana historia kuhusu mambo yaliyotokea tulipokuwa tunapigania uhuru wetu. Tunajua pia kuna Wakenya waliochukuliwa wakati wa nyuma katika Vita Vikuu vya Dunia ama World War, ambao mpaka sasa hawatajwi na hawajulikani. Lakini ikiwa tutahusisha jamii kwa jumla katika jambo hili, itakuwa vizuri. Kwa hakika, wale wakongwe wetu kule mashinani wanaijua historia ya nchi yetu ya Kenya vizuri. Nashukuru sana kwa kunipatia nafasi hii. Nawaomba Wakenya wenzangu tuunge mkono Mswada huu ili hata kesho, kukiwa kuna haja ya kujitolea mhanga, kila Mkenya atajitolea bila kusita. Inafaa kuhakikisha ya kwamba sisi Wakenya tunafikia malengo yetu na azma yetu ili tuwe na nchi ambayo ina mapenzi na maendeleo dhabiti."
}