GET /api/v0.1/hansard/entries/457594/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 457594,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/457594/?format=api",
    "text_counter": 278,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Dr.) Shaban",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 139,
        "legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
        "slug": "naomi-shaban"
    },
    "content": "Ahsante Bw. Spika. Nasimama kuunga mkono Hoja hii baada ya kurekebishwa kwamba mhe. Mututho apewe nafasi ya kufanya kazi ya kupigana na shida hii kubwa humu nchini. Kwetu sisi tunaotoka pwani, hili ni suala la kusikitisha. Watoto wetu kule pwani wanazaa watoto kabla watoto hao hawajafika muda wao. Watoto wanazaliwa wakiwa vilema na matatizo kibao kwa sababu ya matumizi ya mihadarati. Ukienda kule Mkoa wa Kati na hata Mkoa wa Pwani utawakuta vijana wakiwa wamelewa mchana na hawana habari kuhusu yanayoendelea. Tunamtaka mtu kama mhe. Mututho apigane na mihadarati na pombe nchini Kenya. Haiwezekani kumkataza kazi na hali tunamsifu kwa kazi nzuri aliyoifanya akiwa Bungeni kupitia sheria aliyoleta dhidi ya shida kubwa iliyotukabili humu nchini. Sisi tumemwona hata kule vijijini akiangalia kunaendelea nini. Ningependa kuwaambia wenzangu kwamba mhe. Mututho hata kabla hajateuliwa kwa wadhifa huu alipitia kule kijijini kwangu Taveta kuangalia ni njia zipi zinatumiwa kupitisha pombe haramu ambayo inaumiza watu. Vile vile, anaelewa njia za kupitisha"
}