GET /api/v0.1/hansard/entries/457938/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 457938,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/457938/?format=api",
    "text_counter": 214,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwaura",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13129,
        "legal_name": "Isaac Maigua Mwaura",
        "slug": "isaac-mwaura"
    },
    "content": "Ahsante sana, Bi. Naibu Spika wa Muda. Ningependa kusimama na kuunga mkono Hoja hii ambayo inaweza kuhakikisha kwamba akina mama na vijana wanapata nafasi ya kuweza kutumia fedha ambazo zimetengwa na Bunge hili na Serikali kwa miradi ya biashara. Jambo ambalo linafurahisha ni kwamba watu walemavu pia wataweza kuakilishwa katika ile bodi ya kitaifa kupitia baraza la kitaifa kuhusu watu walemavu na pia katika eneo Bunge ambapo mojawapo wa wale ambao watakuwa ni wanakamati atakuwa ni mtu mlemavu ambaye atateuliwa na mashirika ya watu walemavu katika kiwango hicho. Hili ni jambo la kufurahisha kwa sababu ukiangalia maeneo yetu, kila gatuzi linajaribu kuwekeza ndiposa kuwe na watu ambao wataweza kushiriki katika masoko yao. Lakini jambo ambalo pengine ni la kushangaza ni kwamba watu wetu hawana hela mifukoni. Watu wetu bado ni fukara, hawajaweza kujihusisha katika biashara kwa sababu imekuwa ni vigumu sana kupata fedha za kuendeleza zile ajenda ambazo wako nazo, yale mawazo ambayo yataweza kuwafaidi."
}