GET /api/v0.1/hansard/entries/457939/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 457939,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/457939/?format=api",
"text_counter": 215,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwaura",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13129,
"legal_name": "Isaac Maigua Mwaura",
"slug": "isaac-mwaura"
},
"content": "Naunga mkono Hoja hii kwa sababu inaimarisha vile ambavyo tunaweza kujiendeleza, ukianagalia vizuri kabisa. Lakini, pia kuna dosari kwa sababu sijui kwangu mimi kama ingelikuwa bora Hoja hii ipendekeze ule mfuko wa fedha wa akina mama na ule wa vijana uweze kujumulishwa. Wale ambao wamekuwa wakiendesha mifuko hiyo wamekuwa na ujuzi na wamepata maarifa kutokana na vile ambavyo wamekuwa wakiendesha shughuli hizo. Ndiposa tusifanye yale makosa pengine ambayo waliyafanya. Kwa mfano, wanaweza kueleza kinaga ubaga zile changamoto ambazo vijana, akina mama na watu walemavu wanapitia katika shughuli zao za kibiashara. Ninatumaini kwamba kama Bunge tutahakikisha kwamba haya maarifa yanaweza kusaidia ili kuimarisha utekelezaji wa mfuko huu. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}