GET /api/v0.1/hansard/entries/458865/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 458865,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/458865/?format=api",
"text_counter": 21,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Leshoomo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 379,
"legal_name": "Maison Leshoomo",
"slug": "maison-leshoomo"
},
"content": "Bi. Naibu wa Spika, kwa idhini ya Kipengele 44(2)(c) cha kanuni za Bunge, ningependa kuomba taarifa kutoka kwa mwenyekiti wa Kamati ya Usalama kuhusu kuzorota kwa usalama katika eneo la Samburu. Wizi wa mifugo umezidi huko Samburu. Watu wameuawa kwa njia isiyoeleweka. Hali ya usalama imezorota huko Samburu kwa sababu ya wizi wa ng’ombe na hii imechangiwa na biashara haramu ya hao mifugo. Kwa mfano tarehe 26 Oktoba, 2013 ng’ombe 23 walipatikana wakiwa wamebebwa kwenye lori. Mifugo hao walikuwa wakienda kuuzwa. Suala hili lilihusisha maafisa wa usalama. Katika taarifa hiyo ningependa nielezwe yafuatayo:- (i) mpango gani Serikali iko nao ili kumaliza huu wizi wa mifugo; (ii) ni lini mifugo hao watarudishwa kwa wenyewe; (iii) ni hatua gani itachukuliwa kwa wale wanaofanya biashara hiyo haramu; (iv) uchunguzi wa mauaji ya kijana na afisa wa usalama utafanywa lini; na, (v) afisa mkuu wa Idara ya Polisi katika eneo hilo na kamanda wa stesheni husika wataondolewa lini katika sehemu hizo, ama watachukuliwa hatua gani."
}