GET /api/v0.1/hansard/entries/458867/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 458867,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/458867/?format=api",
"text_counter": 23,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Abongotum",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 165,
"legal_name": "Asman Abongutum Kamama",
"slug": "asman-kamama"
},
"content": "Niko hapa, mhe. Naibu wa Spika. Kwanza, ningependa kukubaliana na mhe. Leshoomo kwamba hali ya usalama katika Wilaya ya Samburu imezorota, na haswa katika Wilaya ya Baragoi Kaskazini. Ninafahamu kwamba kuna operesheni inayoendelea katika wilaya hiyo, ya kuwanyanganya bunduki watu wanaozimiliki kwa njia haramu. Kuna askari karibu 700 ambao wanafanya kazi hiyo. Kwa hivyo, ningependa kumhakikishia mheshimiwa kwamba operesheni hiyo inawalenga wakora. Tunajua kwamba kule Baragoi kuna bunduki zaidi ya 46 zilizoibwa na majambazi askari wetu walipouawa kwenye tukio la hapo awali. Tungependa wale askari wanaofanya operesheni hiyo waokoe bunduki hizo kwanza. Pili, kuna operesheni inayowalenga walinzi kutoka kitengo cha KPR. Si jambo la busara kukifutilia mbali kitengo hicho cha walinzi bila ya kuwahakikishia wananchi usalama wa kutosha. Kwa hivyo, operesheni ya kwanza inalenga kuziokoa bunduki za serikali zilizoibwa na majambazi. Kuhusu masuala yaliyosalia, nitaongea na Katibu anayesimamia masuala ya usalama ili tuweze kupata habari kamili kuhusu OCPD na OCS kwa sababu tunajua kwamba kulikuwa na shida iliyotokea kati ya maafisa hao wawili na wanafunzi. Kuhusu suala la ngo’mbe 26 walioibiwa, nitaleta taarifa Bungeni baada ya wiki moja. Ahsante, Bi. Naibu wa Spika."
}