GET /api/v0.1/hansard/entries/460035/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 460035,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/460035/?format=api",
"text_counter": 184,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. S.A. Ali",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2100,
"legal_name": "Shariff Athman Ali",
"slug": "shariff-athman-ali"
},
"content": "Asante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda. Tunaelewa vyema kwamba tuko na Katiba katika nchi hii ambayo sisi kama wananchi tunafaa kuifuata. Vile vile, Serikali inafaa kuifuata hii Katiba. Masikitiko makubwa ni kwamba hali hii inatushangaza sana sisi Waislamu; kwamba yeyote anayeonekana kuwa na imani thabiti kuhusu dini yake, ndiye ambaye anafuatwa katika masuala haya ya mauaji. Mauaji yanapotokea, ni swala ambalo wengi wanajiuliza ni kwa nini jambo hili linafanyika. Hii ni kwa sababu tunaelewa vyema kwamba kuna sheria katika nchi hii. Serikali imejitenga na kusema kwamba haijui watu wote ambao walitajwa na Mhe. Nassir katika mauji hayo, ilhali karibu watu hawa wote wameuawa ama wamekufa katika hali ya kutatanisha. Kwa hivyo, sisi kama Wakenya na Waislamu katika nchi hii tuna haki zetu. Serikali inaponyamaza na kusema kwamba haijui na inahitaji wenye ushahidi waje na ilhali inaonekana wazi kwamba mauaji haya ni ya kupangwa kutokana na hisia za watu hao katika dini, ningependa kupata maelezo kamili kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama wa Kitaifa. Serikali haiwezi kusema kwamba haijui mambo yaya. Ikiwa haijui, inafaa ijitahidi kwa sababu hawa ni Wakenya. Inafaa Serikali itueleze ni vipi watu hawa wamefika katika hali hii. Hii imekuwa ni tishio kubwa kwa Waislamu kwa sababu unaposimama kwa msimamo wako wa kidini, unaonekana kwamba wewe ni terrorist. Na ilhali katika masuala ya terrorist, maelezo au ufafanuzi wa terrorist hauambatani na Uislamu. Terrorist anaweza kuwa ni mtu yeyote katika nchi hii au ulimwengu huu. Mtu yeyote ambaye ako katika dini yeyote anaweza kuwa terrorist. Kwa hivyo, haimanishi kwamba terrorist ni Muislamu peke yake."
}