GET /api/v0.1/hansard/entries/460510/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 460510,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/460510/?format=api",
"text_counter": 330,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Kombe",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 250,
"legal_name": "Harrison Garama Kombe",
"slug": "harrison-kombe"
},
"content": "Mhe. Spika, kazi inayoendelea kwa wakati huu ni kazi ambayo inaridhisha. Wengi wetu tulikuwa hatujajua rangi ya cheti cha kumiliki shamba. Lakini imefikia wakati yale mashamba ambayo yalikuwa yamekaliwa miaka na miaka kupatiwa wenyewe. Kuna wengine hapa Kibera tu. Kulikuwa na shamba la Wanubi ambalo limekaa miaka na miaka. Kila mwaka, lakatwa kipande mpaka sasa limebakia ekari 400. Nakumbuka siku moja Waziri alikuja akatuambia kwamba atafanya juu chini kuhakikisha kwamba Wanubi wanapata ardhi hiyo, hata kama itabidi kuuma risasi. Hiyo ni ishara ya kwamba alikuwa amejitolea kufanya kazi kisawa sawa ili kwamba mambo yaweze kuwa mazuri kwa wale Wakenya wanyonge zaidi. Mhe. Spika, pale alipoingia katika jengo la Ardhi House, ni shimo la tewa. Unaweza ukatafuta hati ya kumiliki ardhi miaka na miaka. Lakini mwenye hela akiingia pale, kwa wiki moja, atatoka na hati ya kumiliki ardhi. Hiyo ndio kazi huyu mama amejitolea kufanya na kulisafisha lile jumba. Lakini hilo halionekani. Mhe. Spika, tusipokuwa waangalifu, tutaiangamiza nchi hii. Kwa hakika, twendeni mbele tukiangalia tunapotoka. Wengi wamekalia Wizara hiyo lakini hatujaona manufaa ila wakati huu. Si kwamba napinga ripoti hii, la hasha! Nina heshima na naipa sifa zote kamati inayosimamia mambo ya ardhi kwa kufanya kazi yake vizuri. Ikiwa lengo la kupitisha ripoti hii ni kumwondoa Waziri huyu, ninaapa hapa kwamba sitakuwa pamoja na huyo atakayeleta Mswada wa kumwondoa. Kwa ndani, watu wanacheka na kufurahia kwa sababu wanajua wamemshika Waziri. Tutayafanya yote hayo lakini ikiwa ni ya kugandamiza wanyonge, hatutakuwa pamoja hata kidogo. Kwa hakika, yote na yawe. Ijapokuwa sina tashwishi na ripoti hii, lakini litakuwa jambo nadra kuiunga mkono. Asante mhe. Spika."
}