GET /api/v0.1/hansard/entries/460831/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 460831,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/460831/?format=api",
    "text_counter": 223,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Wario",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 252,
        "legal_name": "Ali Wario",
        "slug": "ali-wario"
    },
    "content": "Asante Mhe. Spika. Ninachukuwa fursa hii kukushukuru. Wahenga walisema kwamba, “Mnyonge kupata haki ni mwenye nguvu kupenda,” Ninasema hivyo kwa sababu nimesimama katika Bunge hili kuchangia Hoja hii. Kulingana na kipengele 89(3)(d) cha Kanuni za Bunge, kwa heshima na taadhima kubwa, uliahidi na kusema kwamba: “Mhe. Wario, nimesikia nitakuja kuamua.” Siku ya kwanza, ya pili, na ya tatu nimekaa kungojea uamuzi kutoka kwa Mhe. Spika. Kwa sikitiko kubwa sikupata uamuzi huo. Leo nimeambiwa kwamba: “Mhe. Ali Wario, huna habari, uamuzi ulishatolewa.” Ikiwa hivyo ndivyo ilivyo, nimechukua uamuzi wako na wacha niendelee mbele na msafara. Mhe. Spika, ninasema kwamba; tunaambiwa kwamba Halmashauri ya Nafaka na Mazao itakwenda kuzama. Ni lazima tusimame wima tuokoe Halmashauri hiyo isizame. Swala nyeti ni kwamba, wakati zabuni ya kuleta mahindi ilitolewa, ni nani aliitoa kwa M/s Erad Supplies and General Contracts Limited? Ni Halmashauri ya Nafaka na Mazao ndio ilitoa hiyo zabuni bila kuangalia masharti? Mhe. Spika, tunaambiwa kwamba Serikali itafute pesa ipeane kwa Halmashauri ya Nafaka na Mazao na bado viongozi wa Halmashauri ya Nafaka na Mazao ni wale wale!"
}