GET /api/v0.1/hansard/entries/460849/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 460849,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/460849/?format=api",
    "text_counter": 241,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Wario",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 252,
        "legal_name": "Ali Wario",
        "slug": "ali-wario"
    },
    "content": "Bw. Spika, nilipoleta hoja ya nidhamu, niliitwa majina mengi ikiwemo kusemekana kuwa nimeleta hoja kupinga, moja, kwa sababu ya ufisadi na pili, kwa sababu ya ukabila. Mimi nimetoka Mkoa wa Pwani, kisha Pwani barani, si baharini kule. Katika hiyo bara, cheo kubwa kabisa tulichonacho katika Serikali ni DC. Ukabila hautanipeleka mahali. Mimi ni kiongozi na ninatoka Bura ambapo kumetoka makabila 42 ya nchi ya Kenya. Siwezi kuleta hoja kwa ajili ya ukabila. Pendekezo la 13 katika ripoti iliyo mbele yetu linasema uchunguzi ufanywe kwa sababu ukame ambao umetangazwa haufai kutangazwa saa hii. Wajibu wa kutangaza ukame kama janga la kitaifa ni wa nani? Miaka tisa iliyopita, Bunge lilikuwa wapi? Ule ukame uliotangazwa miaka tisa iliyopita, uchunguzi uanze? Tunatumia cheo na mamlaka vibaya."
}