GET /api/v0.1/hansard/entries/460853/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 460853,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/460853/?format=api",
    "text_counter": 245,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Wario",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 252,
        "legal_name": "Ali Wario",
        "slug": "ali-wario"
    },
    "content": "Bwana Spika, pendekezo la 13 linasema kwamba uchunguzi ufanywe katika Wizara ya Miradi Spesheli na Wizara ya Kilimo kwa kutangaza ukame. Miaka tisa imepita sasa. Kwa nini ukame ulitangazwa kuwa janga la kitaifa? Wajibu wa kufanya hivyo ni wajibu wa Baraza la Mawaziri na Rais. Kwa nini ripoti haijaletwa hapa? Ripoti hi inatupatia ukweli nusu na uongo nusu. Hatujaambiwa fedha ni za nani. Tumechukua kampuni moja na kujaribu kuihalalisha kwa sababu tunataka kuwaambia Wakenya kwamba hawa ndio wabaya zaidi. Je, wale waliochukuwa zabuni ya kuleta tani zaidi ya 110 wako wapi? Wamefanya nini? Wamelipwa pesa ngapi? Ripoti hii haituelezi hayo. Kwa sababu kuna Erad, tutaonyeshwa hiyo Erad na ukweli mwingine ufichwe. Tutapitisha hii ripoti kwa ajili ya kufurahisha watu fulani. Tuelezeni Purma ni ya nani? Tueleze Freba ni ya nani? Tueleze Euro Commodities ni ya nani? Wamelipwa hela ngapi? Ukifanya hivyo mimi nitakuamini kisha nikuunge mkono. Bunge hili linapaswa kutoa ukweli na haki kwa Wakenya wote."
}