GET /api/v0.1/hansard/entries/460860/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 460860,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/460860/?format=api",
    "text_counter": 252,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Wario",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 252,
        "legal_name": "Ali Wario",
        "slug": "ali-wario"
    },
    "content": "Bwana Spika, hii ni nyumba ambayo inaangaliwa na Wakenya wote, wakubwa kwa wadogo na watoto kwa wazee. Tegemeo lao ni sheria tunazotunga hapa. Bila usawa na haki hadhi ya nyumba hii itateremka. Kuna pendekezo moja kwamba Serikali itoe ruzuku kwa NCPB ili iweze kusimama. Mimi nitaunga hilo mkono ikiwa viongozi wa NCPB watabadilishwa. Baada ya hukumu kutolewa wale waliokuwepo hawakwenda kukata rufaa. Hawakumjulisha Mkuu wa Sheria kwamba kuna tatizo kama hili. Kwa sababu gani? Ni kwa sababu wao pia wana mikono yao ndani ya suala hili. Ikiwa Erad imepoteza robo ya mali ya umma, NCPB itapoteza theluthi tatu ya mali ya umma. Kwa sababu ya NCPB, ninapinga ripoti iliyomo ndani ya Bunge hili."
}