GET /api/v0.1/hansard/entries/464143/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 464143,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/464143/?format=api",
    "text_counter": 390,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Leshoomo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 379,
        "legal_name": "Maison Leshoomo",
        "slug": "maison-leshoomo"
    },
    "content": "Mhe. Naibu Spika wa Muda, tukio la tarehe 2.10.2013 lilinishangaza sana. Kama alivyoeleza mhe. Lentoimaga, watoto waliuawa na ng’ombe kuibiwa. Jambo la kushangaza ni kwamba ripoti rasmi ya Serikali iliyoletwa Nairobi inasema kwamba hakuna mtu aliyeuawa ama ng’ombe kuibiwa. Ripoti hiyo ilitumwa Nairobi licha ya kwamba maiti za waathiriwa zilikuwa bado hazijazikwa. Hali hiyo inanikera sana. Tulifanya kampeini ya amani miongoni mwa wakazi wa sehemu hiyo, na watu wakarudiana na kuanza kukaa pamoja kwa amani. Hatujui vita vilianzia wapi tena. Swali ambalo ningependa kuuliza ni: Ng’ombe hao wanapelekwa wapi?"
}