GET /api/v0.1/hansard/entries/464649/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 464649,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/464649/?format=api",
    "text_counter": 152,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Gathogo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2715,
        "legal_name": "Esther Nyambura Gathogo",
        "slug": "esther-nyambura-gathogo"
    },
    "content": "Asante sana, Bi. Naibu Spika kwa hayo majibu kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mazingira na Mali ya Asili. Ningetaka kusema kwamba sijaridhika kwa sababu wakulima katika eneo bunge la Ruiru na Kenya yote wanateseka kwa sababu ya hawa wanyama wa pori. Wakati wanyama wameuliwa, tunakimbizwa na watu wanateswa sana kwa sababu ya kuwaua. Wanyama wakiua watu, hakuna malipo wanapata. Kwa hivyo, ninamshukuru Mwenyekiti lakini sijaridhika. Ningetaka kuikaribisha Kamati kwa eneo langu la Bunge. Tuko na bwawa la maji la tatu ambapo tumeuliza Serikali iweke seng’enge ya stima lakini haijawekwa. Wiki iliyopita, mtoto mdogo alikuwa karibu kuumwa na mamba akitoka shule. Kwa hivyo, sitaki kulichukulia jambo hili kwa mzaha na ningetaka kulipata jibu ambalo litaniridhisha. Sijaridhika kamwe!"
}