GET /api/v0.1/hansard/entries/464933/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 464933,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/464933/?format=api",
    "text_counter": 436,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Kipyegon",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1453,
        "legal_name": "Johana Ngeno Kipyegon",
        "slug": "johana-ngeno-kipyegon"
    },
    "content": "Watoto wetu wanaumia shuleni kwa sababu ya utenda kazi duni wa TSC. Ni lazima tubuni tume ya TSC itakayozingatia maslahi ya walimu. Tukizingatia masuala yaliyozungumziwa hapo awali, watu wengi wameuliza iwapo sheria ilifuatwa. Ningependa kusema kwamba wanakamati hao walifuata sheria na kufanya kazi ya maana. Kwa mara ya kwanza katika historia ya Bunge, wameonyesha kwamba Bunge si muhuri wa kupitisha matakwa ya kibinafsi ya watu fulani. Wabunge si ng’ombe wa kupelekwa mtoni na kurudishwa bomani. Sisi ni watu ambao hutekeleza wajibu wetu kwa mujibu wa sheria. Ningependa kusema kwamba mwenyekiti na wanakamati wake walifanya kazi nzuri sana. Hii siyo siasa ya mahali moja ama nyingine."
}