GET /api/v0.1/hansard/entries/464993/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 464993,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/464993/?format=api",
    "text_counter": 496,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Dukicha",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1480,
        "legal_name": "Hassan Abdi Dukicha",
        "slug": "hassan-abdi-dukicha"
    },
    "content": "Ahsante Bw. Naibu Spika wa Muda pamoja na mhe. Chege Sabina. Nataka mnisikize vizuri. Nimengojea hii nafasi kwa muda mrefu. Nimeinua mkono, nimekaa chini--- Nasimama kuunga mkono Hoja hii. Kule Tana River ninakotoka sisi huwa wa mwisho kila mwaka matokeo ya mitihani ya kitaifa inapotokea. Kama si sisi basi ni Lamu. Ikiwa hatutaangazia masuala haya kwa undani Tana River itaangamia na mimi sitakubali kitu kama hicho. Kamati hii imefanya kazi yake vizuri. Sasa kamati itupatie majina ya watu wanaostahili kupata nafasi hizo. Hili si suala la jamii na Wakenya."
}