GET /api/v0.1/hansard/entries/46585/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 46585,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/46585/?format=api",
"text_counter": 328,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Mwakulegwa",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 101,
"legal_name": "Danson Mwazo Mwakulegwa",
"slug": "danson-mwazo"
},
"content": "Ahsante Bw. Naibu wa Spika. Naomba kuunga mkono hoja hii ambayo kupitishwa kwake kutasaidia watu walio na umri wa miaka sitini na zaidi. Watu hawa hupatwa na magonjwa, hukosa chakula, na hawaangaliwi na jamii zao. Huduma za matibabu zimeangamia na kwa hivyo wazee wanapata taabu. Tunaomba Serikali iwapatie msaada huu hawa watu 1.8 milioni. Hawa wazee walizalisha uchumi wa nchi wakiwa na umri mdogo. Sote tutafika umri huo wa miaka 60 na zaidi. Ukifikisha umri huo, usifikirie kwamba umeachwa uende kaburini. Serikali, kuambatana na Katiba mpya, ina jukumu la kuhakikisha kwamba wale wazee wameangaliwa hasa kiafya kwa sababu hali ya matibabu imedidimia mno. Wazee wakipewa pesa hizi, wataweza kujilisha na kujigharamia kimatibabu na kwa hivyo siku zao humu duniani kuongezeka. Vile vile, tunaomba Serikali kwamba itakapoongeza pesa hizo ibuni pesa za kusaidia wazee ambao wana nguvu na uwezo wa kuchukuwa mikopo ili waweze kuendeleza shughuli kama vile kilimo. Wengi wa hawa wazee hurudi mashambani kuendeleza kilimo. Kwa sababu ya msingi wa umri, utapata kwamba mikopo haipeanwi watu walio na umri wa miaka 60 ama 65. Kama kungekuwepo na kiwango cha pesa kilichotengewa hawa wazee walioko mashambani, basi wangeweza kuzalisha mali na kujimudu kifedha. Bw. Naibu wa Spika, sisi hupata shida kule mashinani tunapoulizwa maswali kwa nini Serikali iliamua kwamba katika kila eneo bunge kupeanwe hela katika lokesheni moja. Zikipeanwa katika lokesheni moja katika eneo bunge, sisi wengine tunaonekana ni kama tunapendelea maeneo yetu. Ikiwa kwa bahati mbaya ni lokesheni unayotoka wewe, basi inaonekana wewe ndiwe uliamua watu hawa wasaidiwe kwa sababu wanatoka kwako. Tunaomba katika bajeti ijayo, kiasi cha fedha kiongezwe na zipeanwe wilaya zote ili sisi tusiwe katika hatari ya kuambiwa kwamba tumechagua. Kama sivyo, kila mbunge atakuwa anaulizwa katika kila mkutano na wazee ambao ni baba zake. Kila mara inatubidi kuwaambia kwamba hela zitaongezwa. Tunaomba Waziri anayehusika azingatie hili katika bajeti yake na hela ziongezwe. Hivyo, wazee watapata malipo hayo ili wanapoishi duniani wakingojea siku zao za mwisho wawe na afueni. Waweze kucheka mpaka siku ya mwisho. Katika hizi kaunti 47 ambazo tumebuni, ingekuwa vizuri ikiwa tungewajengea majumba. Hivyo, wazee ambao hawana watu wa kuwalinda kama vile wajukuu ama watoto wao wapate chakula na matibabu. Kwa sasa utapata mzee hana chakula wala mtu wa kumwangalia ama kumsalimia. Kwa hivyo tunaomba Wizara inayohusika ifanye hivyo. Naunga mkono."
}