GET /api/v0.1/hansard/entries/46591/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 46591,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/46591/?format=api",
    "text_counter": 334,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Mashariki hazipati msaada huu. Kwa hivyo, itakuwa ni vizuri kwa Serikali kushughulikia umaskini ambao umekithiri sana katika nchi hii. Kama tunavyojua, mara nyingi Serikali hutumia pesa nyingi kuwanunuliwa watu chakula katika sehemu kame za nchi hii. Msaada huu huwa ni mahindi na maharagwe. Msaada huu hausaidii sana watoto na wazee. Hii ni kwa sababu watu hawa watahitaji vyakula vingine mbali na mahindi na maharagwe ili waimarishe afya yao. Wafugaji wengi wamezoea kula nyama na kunywa maziwa. Hoja hii inapendekeza wazee wasiojiweza wahudumie vizuri. Hii ni kwa sababu utamadumi wa Kiafrika wa kuwasaidia wanyonge na jirani wetu ambao wana shida nyingi, hauzingatiwi tena. Siku hizi watu wengi hawasaidii maskini, mayatima na wajane kwa sababu wao pia wana shida zinazotokana na hali ngumu ya maisha. Bw. Naibu Spika, Jumamosi iliyopita nilizuru Kamukunji Constituency, mtaa wa Bahati. Niliona vijana wengi ambao hawana kazi. Niliona uchungu kuona vijana hawa wamepanda mboga au sukumawiki katika magunia yaliojaa mchanga. Watu wetu wanatafuta kila njia ya kuweza kujisaidia. Wanapanda mimea ya kila aina ili waweze kupata riziki yao ya kila siku. Watu wengi ambao wangependa kuwasaidia jamii yao hawawezi. Hii ni kwa sababu pia wao wana shida zinazotokana na hali ngumu ya uchumi. Hali ya maisha imekuwa ngumu sana, hasa kutokana na upungufu wa mvua. Mifugo yetu imeangamia kwa sababu hakuna malisho ya kutosha. Ikiwa hali itaendelea hivi kufikia mwisho wa mwezi wa Juni, basi umaskini utaongezeka maradufu. Ninaiomba Serikali ifanye lolote kuhakikisha ya kwamba wazee miongoni mwetu ambao hawapati riziki ya kila siku wamepewa pesa hizi. Tukifanya hivyo, basi wazee wetu watafaidika. Kwa hayo machache, ninaunga mkono Hoja hii."
}