GET /api/v0.1/hansard/entries/46592/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 46592,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/46592/?format=api",
"text_counter": 335,
"type": "speech",
"speaker_name": "Ms. Leshomo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 379,
"legal_name": "Maison Leshoomo",
"slug": "maison-leshoomo"
},
"content": "Asante sana, Bw. Naibu Spika kwa kunipa nafasi hii ili niseme machache juu ya Hoja hii. Ninamshukuru Mbunge ambaye ameleta Hoja hii katika Bunge hili. Hii ni kwa sababu wazee wengi wana shida nyingi sana. Ikiwa tutaipitisha Hoja hii, wazee wengi kule mashinani watafaidika. Tumeelezwa kuwa kuna wazee katika nchi hii ambao wamekuwa wakipata msaada huo. Msaada huo umeleta shida kwa viongozi wengi. Wazee wetu ambao hawapati pesa hizi wanadhani sisi hatuwatetei. Ninaunga mkono Hoja hii kwa sababu wazee wengi watafaidika kutokana na pesa hizi. Ninataka pia akina mama wazee nao pia wasaidiwe kwa sababu wana shida nyingi. Pesa hizi zitawasaidia wazee wote katika nchi hii. Iwapo tutaipitisha Hoja hii, ninaiomba Serikali kuitekeleza mara moja. Wazee wa kutoka sehemu kame wanahitaji maziwa na nyama. Mahindi na maharagwe ni ngumu kwao kutafuna kwa sababu hawana meno. Bw. Naibu Spika, wazee wengi kutoka wilaya yetu wamehamia mjini ili wapate msaada kutoka kwa Kanisa la Katoliki. Jumamosi na Jumanne, zaidi ya wazee 400 hungoja chakula cha msaada kutoka kwa kanisa hili. Hii ni kwa sababu kuna umaskini mwingi katika taifa letu. Vijana wengi ambao wangewasaidia wazee hawa hawana kazi na mifugo yetu imekufa kutokana na ukame. Bw. Naibu Spika, mimi ni kama shirika la kusaidia watu wasiojiweza kwa sababu hulisha zaidi ya wazee 250. Watu hawa ni maskini sana. Ninajua pia waheshimiwa Wabunge wengi hapa wanawasaidia watu wengi sana. Kwa hivyo, ni lazima tuipitishe Hoja hii ili wazee wetu wafaidike. Kwa hayo machache, ninaunga mkono Hoja hii."
}