GET /api/v0.1/hansard/entries/465951/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 465951,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/465951/?format=api",
    "text_counter": 498,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwaura",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13129,
        "legal_name": "Isaac Maigua Mwaura",
        "slug": "isaac-mwaura"
    },
    "content": "Mhe Spika wa Muda, hili ni jambo muhimu kwa sababu tunajua kwamba bei ya maisha imeenda juu mno, na pia kwamba kwa sababu ya ile sheria ya VAT ambayo tulipitisha hapa, watu sasa wanaona ni vigumu sana kujimudu. Hata tumeona wale wakulima wa kule Gatundu wakilalamika kwamba bei ya chakula cha mifugo imeongezeka sana, na baina ya mifugo hawa kuna ng’ombe. Bei ya chakula imeongezeka lakini bei ya maziwa ambayo wakulima huuza imebaki chini. Kwa hivyo, ningependa sana kuunga mkono ndiposa pia wao waweze kuhakikisha kwamba hiyo bei haiwaathiri."
}