GET /api/v0.1/hansard/entries/465954/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 465954,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/465954/?format=api",
    "text_counter": 501,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwaura",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13129,
        "legal_name": "Isaac Maigua Mwaura",
        "slug": "isaac-mwaura"
    },
    "content": "Mhe Spika wa Muda, nikimalizia nina kasheshe kidogo kwa sababu hivi karibuni tumeweza kuona kwamba makampuni madogo ya maziwa yameweza kununuliwa na makampuni makubwa, na hivyo basi inaonyesha kwamba soko la maziwa linamilikiwa na watu wachache. Ukiangalia sana utaona tuna New KCC na sasa Brookside kama makapuni ya maziwa yenye uwezo; hili ni jambo ambalo linanitia kiwewe. Katika ile kampuni ambayo inaitwa Githunguri Dairy kule ambako natoka kuna msukumano. Hii itafanya wakulima wasiwe na masoko mengi ya kuuza maziwa yao. Lakini nafikiri afueni itatoka kwa kampuni ya Serikali ambayo inaitwa New KCC, kama vile ambavyo tuna ile tume ya kawi, yaani Energy Regulation Commission, ambayo kila wakati inatuambia bei ya petroli imepanda ama imeshuka."
}